Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa amesikitishwa na mashambulizi yaliyotokea nchini Mali na kuwataka viongozi wa nchi hiyo kudhibiti ghasia za visasi, kulingana na taarifa iliyoelezwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric

Watu takribani 95 waliuawa nchini Mali siku ya Jumatatu wakati watu wenye silaha waliposhambulia kijiji kimoja usiku kucha kwa kuwafyatulia watu risasi pamoja na kuchoma moto nyumba zao. amesema msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Mali, Amadou Sangho

Mivutano imekuwepo nchini humo kwa miaka kadhaa kati ya wakulima wa kabila la Dogon na wafugaji wa kabila la Fulani, ambapo machi 23 takribani watu 160 wa kabila la Fulani waliuawa wakati watu wenye silaha waliposhambulia kijiji cha Ogossagou katika eneo hilo hilo, huku Wakulima wa kabila la Dogon walituhumiwa kufanya shambulio hilo.

Mjumbe wa kundi linaloangalia matatizo ya kimataifa, Jean-Herve Jezequel aliandika katika ripoti yake baada ya mauaji ya mwezi Machi kwamba wakulima hao wamekuwa kundi la wanamgambo wenye silaha wakieleza kwamba wanahitaji kuilinda jamii yao kama vikosi vya usalama vya Mali haviwezi kufanya hivyo.

Jean-Herve Jezequel alieleza kwenye ripoti hiyo kwamba kuwepo silaha za kivita na nia ya wapiganaji wa makundi ya jihadi yamefungua milango ya viwango tofauti vya ghasia zinazohusu makabila.

 

Video: Magufuli aagiza fagiafagia TRA, Darasa la saba waitwa JKT
LIVE: Yanayojiri Bungeni Jijini Dodoma