Mapigano nchini Sudan, yanaripotiwa kupungua kasi, ingawa bado yanaendelea huku suala la usitishaji mapigano ambalo likiibua matumaini yenye tahadhari ambapo njia za misaada na barabara zinazotumika kwa ajili ya kukimbia vita zikitarajia kufunguliwa hivi karibuni.
Hata hivyo, mashambulizi ya anga na mashambulizi ya silaha bado yameendelea kusikika jijini Khartoum, huku waangalizi wa Marekani na Saudi Arabia wakisema mapigano hayo yanaonekana kupungua tangu kuimarishwa kwa sitisho la wiki moja.
Aidha, Maafisa wa Washington na Riyadh ambao walisimamia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya vikosi vya majenerali wawili hasimu, walielezea kwenye ripoti yao kuakiashiria pande zote mbili zilikiuka maazimio ya usuluhishi.
Hata hivyo, wasuluhishi hao wanasisitiza kuwa maandalizi yanaendelea kupeleka misaada ya kuokoa maisha kwa watu wa Sudan ambao wamevumilia zaidi ya wiki tano za mapigano ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.