Kiungo Mshambuliaji kutoka England Bukayo Saka ametia saini mkataba mpya wa kubakia Arsenal hadi mwaka 2027, akisema klabu hiyo ndipo sehemu sahihi ya kupiga hatua inayofuata.

Mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa ya England amefunga mabao 14 kwa Washika Bunduki hao msimu huu, na kutoa pasi 11 za mabao.

Akiwa na umri wa miaka 21 tu, tayari ameichezea klabu hiyo mechi 178 na ameshiriki katika mechi zote za Ligi Kuu England katika kipindi cha mismu miwili iliyopita.

“Nimefurahi sana tu,” amesema Saka.

“Kumekuwa na mazungumzo mengi na muda umepita, lakini niko hapa sasa. Nadhani hii ni klabu sahihi, mahali pazuri kupiga hatua inayofuata. Ni klabu nzuri, angalia tulipo.

“Kwangu mimi, ni juu ya kufikia malengo yangu binafsi kiasi gani ninajisukuma na kudai kutoka kwangu kila mchezo, wiki baada ya wiki.

“Halafu nina watu wote wanaofaakaribu nami katika suala la familia, na ninapokuja kwenye mafunzo, wachezaji wenzangu na wafanyakazi wananipa ushirikiano mkubwa.

“Nadhani nina kila kitu ninachohitaji ili niwe mchezaji bora zaidi, ninaweza kuwa, na ndiyo sababu nina furaha kubaki hapa na kuwa hapa kwa siku zijazo, kwa sababu ninaamini tunaweza kufikia mambo makubwa.”

West Ham Utd kuzitega Arsenal, Man Utd
Hakuna dalili za kusitishwa kwa mapigano Sudan