Harry Kane alifunga mabao mawili katika mchezo wa ligi ya mabigwa Ulaya uliopigwa katika uwanja wa Wembley ambapo Tottenham wameanza vizuri michuano hiyo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Borussia Dortmund.

Spurs walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Heung-Min Son dakika nne tu baada ya mchezo huo kuanza lakini Andriy Yarmolenko aliisawazishia Dortimund bao hilo dakika ya 11.

Dortmund walitawala mchezo katika kipindi cha kwanza huku Christian Pulisic na Pierre-Emerick Aubameyang wakifunga mabao ambayo hatahivyo yalikataliwa kwa kuwa waliotea.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane alianza kuzifumania nyavu dakika ya 15 akifunga bao la pili baada ya Tottenham kufanya shambulio la kushtukiza akipachika mpira wavuni kwa mtindo unaofafana na ule wa Heung-Min Son.

Kane aliiweka mbele zaidi Tottenham baada ya kufunga bao tatu dakika ya 60 kufuatia kazi nzuri ya Christian Eriksen na Ben Davies na kufanya dakika 90 kumalizika kwa Spurs kuwapiga Dortimund kwa mabao 3-1.

Son akishangilia baada ya kufunga bao

Katika mchezo huo Spurs walijikuta wakimaliza wakiwa kumi uwanjani baa ya mchezaji Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu.

 

 

Mwanasiasa maarufu atekwa nchini Burundi
Ni zamu ya Paris na Los Angeles Olimpiki 2024, 2028