Kocha mpya wa Tottenham, Ange Postecoglou alishikwa na hasira akiwa katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kuulizwa kuhusu mustakabali wa Nahodha na Mshambuliaji Harry Kane, huku klabu hiyo ikiendelea kutoa utetezi.
Postecoglou hakufurahishwa wakati mwandishi wa gazeti la Ujerumani alipoonyesha jezi ya Bayern Munich yenye jina la Kane kwenye mahojiano yaliyoanza kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Leicester uliyochezwa jana Jumapili (Julai 23), jijini Bangkok.
Mbali na kuonyesha jezi hiyo, mwanahabari huyo alimwambia kocha huyo raia wa Australia: “Hiyo inaonekanaje?’ kisha alicheka na kuuliza; “Inaonekana vizuri, au hapana?”
Kutokana na swali hilo, alifoka kwa Postecoglou hasira kali: “Sijui unazungumzia nini. Naona unafurahi kabisa? Vizuri sana. Umefika mbali sana.”
Hivi karibuni kocha huyo alishindwa kuzungumzia uvumi wa Kane huku Bayern ikiwa tayari imetoa ofa mbili ambazo hata hivyo zilipigwa chini.
Hata hivyo, klabu yake ilitetea kuhusu hatma ya Kane wakikana madai ya kuondoka kwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya England.
Spurs imefanya ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya Australia na Kusini Mashariki mwa Asia na imekuwa kama mwenyeji huko kwa sababu mara nyingi wanafanya ziara kwenye nchi hiyo kipindi cha Pre Season, huku baadhi ya wachezaji wakishiriki kwenye masuala ya kijamii akiwamo Heung-min Son, Ivan Perisic, Joe Rodon na Pape Matar Sarr.
Spurs imekodisha ndege itakayobeba kikosi na wafanyakazi wote katika ziara hizo, ikisafiri moja kwa moja hadi Australia.