Inaelezwa kuwa kikao kati ya mabosi wa Bayern Munich na mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs kilienda vizuri na kwa sasa vigogo hao wa Munich wanajiandaa kuwasilisha ofa nono ambayo itaenda kuvunja rekodi yao ya usajili na kumfanya Kane kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kutokea kwenye viunga vya Munich.

Taarifa kutoka Sky Sports zinaeleza Munich ipo tayari kutoa Pauni 100 milioni ambayo inahitajika na Spurs ili kuipata huduma ya Kane.

Mchezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Bayern hadi sasa ni Lucas Hernandez ambaye zilitumika Pauni 68 milioni kumchukua akitokea Atletico Madrid.

Kane ambaye alipewa ofa ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Spurs kwa kuwa mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu, alikataa na kusisitiza anahitaji kuondoka.

Hatma yake inadaiwa kuamuliwa kwenye kikao cha mwisho kilichofanyika jana Jumanne (Agosti Mosi) na inaelezwa Spurs wapo tayari kumuuza lakini sio chini ya Pauni 100 milioni.

DCEA, JKT Ruvu wateketeza mashamba ya Bangi
Maxi Mpia avuruga hesabu kikosini