Haruna Niyonzima Hakizimana anaachana na Young Africans rasmi baada ya msimu huu kufikia tamati.
Leo Alhamisi (Julai 15) kiungo huyo kutoka Rwanda ameagwa na viongozi na wachezaji wenzake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu FC katika uwanja wa Mkapa ikiwa ndio mchezo wa mwisho wa msimu kwa Young Africans kucheza nyumbani Dar es salaam.
Niyonzima mchezaji bora na kipenzi asiye Mtanzania kuwahi kuvaa jezi ya Wananchi, ameichezea Young Africans kwa miaka minane, akishinda mataji Manne ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Taji moja la Kombe la Shirikisho la Azam, Kombe la Ngao ya Jamii mara tatu, Mapinduzi Cup mara moja na Ubingwa mara Moja wa CECAFA Kagame Cup.
Alikuwa mmoja wa wachezaji wa Young Africans walioweka historia ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mnamo 2016.
Alirejea kwa mara ya pili kuwatumikia Wananchi mwaka 2019 kutoka AS Kigali ya kwao Rwanda, Niyonzima pia alishinda misimu miwili kwa watani zao, Simba SC kati ya 2017 hadi 2019 kwa mafanikio ambapo makubwa ni kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe hatostaafu soka lakini atandelea kuutumikia mpira kwa kuendelea kucheza.