Michezo tisa yote iliyopigwa leo imemalizika kwa huzuni, furaha na matumaini kwa mbalimbali… furaha kubwa ilianzia kwa Biashara United ambao wamejihakikishia kumaliza msimu nafasi ya nne na rasmi wao ndio wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao 2021-22 na Young Africans itamaliza nafasi ya pili hivyo kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Huzuni kubwa kwa leo, imeenda kwa Ihefu (mchezo wa mwisho vs. KMC) , Gwambina (vs. Prisons) na JKT Tanzania (vs. Mtibwa) ambapo vipigo hivi kwao vinamaanisha wana nafasi moja tu ya kushinda mchezo wa mwisho wa msimu kwa mabao mengi tu na kuwaombea vipigo vya mabao mengi tu wapinzani wao wa juu ili wao wakacheze playoff ya kubaki VPL na sio matokeo mengine watahitaji zaidi ya ushindi tu.

Coastal Union (Mchezo wao wa mwisho vs. Kagera) waibua matumaini ya kubaki VPL kwa kuhitaji alama tatu mchezo wa mwisho wakati Mtibwa atataka sare tu ili acheze walau Playoff.

FT: Young Africans 2-0 Ihefu SC
[Feisal Salum ⚽⚽]

FT: KMC FC 5-2 JKT Tanzania
[Sadalla ⚽⚽, Ilanfya ⚽⚽, Buyoya ⚽ | Lyanga ⚽, Bilal ⚽]

FT: Ruvu Shooting 2-1 Namungo FC
[David Richard âš½, Fully Maganga âš½ || Reliants Lusajo âš½]

FT: Tanzania Prisons 1-1 Biashara United
[Mohammed Mkopi âš½ | Christian Zigah âš½]

FT: Coastal Union 5-0 Mwadui FC
[Chambo ⚽, Abushehe ⚽, Raizin ⚽, Mudhathir ⚽⚽]

FT: Polisi Tanzania 0-1 Kagera Sugar
[Hassan Mwaterema âš½]

FT: Mbeya City 1-0 Gwambina FC
[Kibu Denis âš½]

FT: Dodoma Jiji 0-0 Mtibwa Sugar

FT: Azam FC 1-1 Simba SC ( Iddy Naldoâš½ | Kagere âš½)

Makamu wa Rais: Tutaimarisha zaidi sekta ya 'NISHATI'
Haruna Niyonzima aagwa rasmi Young Africans