Bondia Hassan Mwakinyo ametoa ufafanuzi wa taarifa zinazoendelea kushika hatamu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuvuliwa Ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBF Intercontinetal).

Juma lililopita Mwakinyo na Ibrahim Class walitajwa kuvuliwa ubingwa wa dunia wa WBF, huku Rais wa Shirikisho hilo Howard Goldberg, raia wa Afrika Kusini, akithibitisha kuvuliwa ubingwa kwa mabondia hao.

Mwakinyo amesema yeye na uongozi wake haujui chochote zaidi ya kudai kuonewa wivu, kwa kuzingatia kanuni inayotamka kuwa bondia akishindwa kutetea ubingwa wake ndani ya miezi sita tangu aupate, basi atavuliwa.

Mwakinyo ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kujibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa watu wanatakiwa wapuuzie suala hilo, kwa kuwa hajui kitu chochote kama mhusika kutokana na kutokupewa taarifa yoyote huku akienda mbali akiamini ni suala la yeye kuonewa wivu na baadhi ya vyombo vikubwa vya habari nchini.

“Puuzeni hizo stori za kuvuliwa mkanda, mimi mhusika na timu yangu hatuna hizo taarifa, watu wasipate uthubutu wa kudanganya umma bila wahusika wa timu kuhakiki na kama ni kweli,”.

Hospitali za mipakani kutoa huduma za kibingwa
Adele aipiga chini show yake