Uongozi wa Simba SC umebainisha kuwa kwa namna wachezaji wao walivyo na shauku ya kufunga mabao mengi kwenye kila mechi wanazocheza ndani ya ligi, huku wakiwa na imani tuzo ya kiatu bora itakuwa kwenye mikono yao msimu wa 2023/24.

Kauli hiyo ni kama kumpora kiatu cha ufungaji bora mwamba Aziz Ki ambaye kwa sasa ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao sita kibindoni baada ya kucheza mechi sita.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/2 3 ni Fiston Mayele wa Young Africans na Saido Ntibanzokiza wa Simba SC walikomba tuzo hiyo baada ya wote wawili kutupia kambani jumla ya mabao 17.

Mayele kwa sasa hayupo Tanzania baada ya kutimkia zake Misri katika Klabu ya Pyramids huku Ntibazonkiza akiwa ndani ya Simba SC akiendelea kupambania kombe akiwa katupia mabao mawili.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kiatu cha ufungaji bora kikawa mikononi mwa Jean Baleke.

“Unaiona kasi ya mshambuliaji Jean Baleke kwenye kufunga mabao jinsi ilivyo? Haishangazi hii ni kazi anayoipenda na usisahau kuwa ana hat trick aliyoifunga kwenye Uwanja wa Uhuru dhidi ya Coastal Union.

“Waanze kumuandalia kiatu cha ufungaji bora mabao matano sasa, ana kasi, uwezo na anapenda kufunga akiwa langoni hivyo huu ni mwanzo mwisho unakuja watafurahi zaidi,” amesema Ally

Wahimizwa usimamizi kuhimili athari mabadiliko Tabianchi
Arteta amkingia kifua David Raya, aponda uchambuzi