Kiungo wa Arsenal, Declan Rice, amesema anajivunia morali na upambanaji wa kikosi hicho baada ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, uliopigwa mwishoni mwa juma lililopita (Jumamosi-Oktoba 21).

Cole Palmer aliwaweka mbele “The Blues’ kwa mkwaju wa Penati, huku shuti kali la Mykhailo Mudryk likiifanya Chelsea kuwa na uongozi wa mabao 2-0.

Rice aliirudisha mchezoni Arsenal baada ya kutumia pasi ya makosa ya Mlinda Lango wa Chelsea, Robert Sanchez, kwa kufunga bao kwa shuti kali, kabla ya Leandro Trossard kuisawazishia dakika ya 84.

Baada ya mechi hiyo, Rice aliwasifu wachezaji wenzake kwa pambano lao la kupata pointi dakika za mwisho kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Akizungumza na Sky Sports, alisema: “Kipindi cha kwanza kutoka kwetu kilikuwa ni kibaya zaidi ambacho tumecheza msimu huu katika suala la uzembe.

“Lakini sifa kubwa kwa Chelsea, kocha wetu alisema hawakuwa na bahati msimu huu na walifanya iwe ngumu kwetu.

“Ili kuonesha moyo na morali, si rahisi wakati upo nyuma kwa mabao 2-0. Ni juu ya kuwa na vita na mawazo, kusukumna timu na kuhakikisha kila mtu ana imani. Ilikuwa kurudi vizuri.

“Chelsea walifanya jambo gumu, lakini sisi kwenye mpira hatukuwa wazuri vya kutosha pasi yangu ya kwanza niliitoa. Iliwapa moyo Chelsea, lakini kipindi cha pili tulionesha tunachokihusu njaa na morali ya kusema haijafika mwisho hadi ifike mwisho. Tulionesha moyo mkuu na morali.”

Rice alifunga bao muhimu ili kuamsha urejesho na anadai kumaliza kwake ilikuwa onesho la silika ya haraka.

Alisema: “Badala ya kuona mpra ukija kwangu nililazimika kukunjuka kwa shuti kali.

“Ilikuwa silika ya haraka kuhusu kupasisha mpira kwa mtu au kuuchukua. Nilikuwa nikipiga kelele, lakini bado tulikuwa chini kwa mabao 2-1 na nilitaka tuendelee na kupata jingine. Nina furaha tulifanya hivyo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 25, 2023
Hassan Dilunga anajitafuta, atajipata