Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 25 oktoba 2021 amekutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa na Mitaji ya Maendeleo UNSDF, Preeti Sinha, Ikulu Dae es Salaam.
Katika taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari, Sinha amemuelezea Rais Samia kuwa UNSDF ipo tayari kushirikiana na nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania kutafuta njia mbadala za kupata fedha za kugharamia miradi ya maendeleo.
Sinha ameongeza kuwa kupitia Mradi wao ujulikanao kama Municiapal Investiment Financing, unaweza kusaidia upatikanaji wa fedha kwa Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Rais Samia, amekubali wazo hilo na kuongeza kuwa litasaidia kupunguza mzigo kwa Serikali Kuu kuhudumia Miradi ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa.
Katika hatua hiyo, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kufanya uratibu utakaowezesha mpango huo kuanza kutekelezwa mara moja.