Maelfu ya raia wa nchini Iran, wameshiriki katika ibada ya mazishi iliyoandaliwa na Serikali kwa ajili ya kuwapumzisha wanajeshi 400 waliouawa katika vita kati ya Iran na Iraq vilivyotokea miaka ya 1980.
Katika ibada hiyo, hisia za athari za vita hivyo zilijionesha kwa familia za wahanga ambao wanasubiri kujua taarifa za ndugu zao ambao hawakurudi kutoka vitani, ambapo majeneza ya askari wasiojulikana yaliyofunikwa kwa bendera ya Iran yalibebwa na kutembezwa kwenye maandamano.
Januari 2022, wanajeshi wengine 250 waliouawa katika vita na Iraq walipewa mazishi kama haya ya kitaifa na katika ibada hiyo Rais wa Iran, Ebrahim Raisi amewatuhumu Marekani na washirika wake kuchochea maandamano dhidi ya serikali ambayo yameendelea kwa takribani miezi mitatu.
Hata hivyo, maandamano hayo yalianza kufuatia kifo cha msichana wa Kikurdi Mahsa Amini kilichotokea mikononi mwa Polisi wa maadili na Waandamanaji zaidi ya 500 wameuawa katika vuguvugu hilo, huku wengine 18,500 wakikamatwa.