Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi, amewasisitizia viongozi wa timu hiyo, kuwa anahitaji kiungo mshambuliaji mwenye uwezo na uzoefu mkubwa wa kucheza michuano ya kimataifa.

Young Africans ambayo msimu ujao itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika, imepanga kukiimarisha kikosi chao ili kifanye vema ikiwemo kucheza Fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Wapo wachezaji wanaotajwa kusajiliwa na Young Africans wanaocheza nafasi ya kiungo mshambuliaji namba 10 ni Fabrice Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyetimkia Azam FC.

Kocha Nabi amesema anahitaji kiungo huyo mshambuliaji mbunifu mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake.

Nabi amesema kuwa anaamini kama akimpata kiungo wa aina hiyo, basi timu yake itafanya vema katika michunano ya kimataifa baada ya msimu huu kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Ameongeza kuwa anaamini msimu ujaoutakuwa mgumu kwao katika michuano ya kimataifa kutokana na mafanikio makubwa wameyapata ikiwemo kucheza Fainali hiyo shirikisho.

“Ninaamini msimu ujao utakuwa mgumu kwetu kwa kuanzia katika Ligi Kuu Bara hadi Ligi ya Mabingwa Afrika, kutokana na mafanikio makubwa ambayo tumeyapata msimu huu.

“Hivyo ni lazima tujipange kwa ajili ya ushindani kwa kuhakikisha tunafanya usajili mkubwa wa wachezaji wenye ubora, uwezo na uzoefu wa michuano ya kimataifa.

“Tayari nimewasisitizia viongozi kuwa, ni lazima tufanye usajili wa kiungo mshambuliaji namba 10 anayemudu kuicheza nafasi hiyo vizuri,” amesema Nabi

Mama asimulia mauaji mke wa Mwenyekiti Bukoba
Uteuzi: Katibu Mkuu TAMISEMI, Mtendaji Mkuu TANROAD