Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), leo Novemba 21, 2020, limetangaza matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi (PSLE), uliofanyika Oktoba 7 na 8, 2020.
Akitangaza Matokeo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 833,672 sawa na asilimia 82.68 kati ya 1,008,307 waliotunukiwa matokeo wamefaulu.
Kati ya watahiniwa hao wasichana ni 430,755 ambao ni sawa na asilimia 82.24 ya wasichana 523,760 waliosajiliwa na wavulana ni 402,917 sawa na asilimia 83.15 ya wavulana 484,547 waliosajiliwa, hili likiwa ni ongezeko la asilimia 1.18 ukulinganisha na ufaulu wa mwaka 2019 ambapo waliofaulu walikuwa ni asilimia 81.50.
Aidha, Baraza la mitihani pia limezifutia matokeo shule 38 za msingi kutokana na udanganyifu uliofanyika wakati wa mitihani ya taifa ya darasa la saba.
Bonyeze link hapa chini kupata matokeo ya Darasa la 7 (PSLE), 2020.