Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, umeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kutwaa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ ambalo lipo mikononi mwao kwa sasa.

Timu hiyo ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa Penati dhidi ya Coastal Union ya Tanga iliyokuwa inanolewa na Juma Mgunda ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha Simba SC.

Young Africans itacheza hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Singida Big Stars, Uwanja wa CCM Liti na mshindi wa mchezo huo atakutana na Azam FC iliyopenya mbele ya Simba SC, mchezo uliochezwa Nangwanda, Sijaona mkoani Mtwara.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kila taji wanalotetea ni muhimu kulirejesha tena kwenye himaya yao.

“Tunatetea Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, hili ni kubwa na muhimu kwetu kulichukua kwa mara nyingine tena na inawezekana kwa kuwa tupo hatua ya nusu fainali.

“Ambacho tutakifanya ni kupambana na kucheza kwa umakini kwenye mchezo wetu wa nusu fainali dhidi ya Singida Big Stars, hiyo itatupa nguvu kusonga mbele hatua ya fainali na kutetea taji letu.” amesema Kamwe.

Dkt. Musa ataka migogoro vyama vya ushirika itatuliwe
Muithiopia kuikamua Simba SC Milioni 300