Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2019-2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani Tsh. 113.5 bilioni.
Akizungumza na wanahabari leo Mkurugenzi Mtendaji wa HELSBÂ Abdul-Razaq Badru amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).
Ambapo katika mwaka huu wa masomo serikali imetenga Tsh.450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha wanafunzi 128,285 kati ya hao zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo.
Aidha, 2018/2019 fedha zilizotengwa na kutolewa zilikuwa Tsh. 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.
Mkurugenzi huyo amesema katika utoaji wa mikopo hiyo wamezingatia vigezo mbalimbali na kuwapa kipaumbele wenye uhitaji maalum kama vile walemavu, yatima, wanaishi katika mazingira ya umasikini haswa wale wanaosaidiwa na Tasaf.