Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), Abdul-Razaq Badru amesema wameongeza bajeti ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 kwa asilimia 14.7 ambalo limefikia Shilingi 654 bilioni kutoka Shilingi 570 bilioni za awali.
Badru ameyasema hayo hii leo nakuongeza kuwa kiasi hicho cha fedha kitawezesha wanafunzi 28,000 kupata mikopo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa masomo.
Amesema, ha kufikia sasa jumla ya wanafunzi 166,438 wamepangiwa mikopo kiasi cha Shilingi 424.5 bilioni na kati yao Wanafunzi wa mwaka wa kwanza ni 68,460 na Wanafunzi 97,978 ni wale wanaoendelea huku walengwa wakiwa 71,000.
Hata hivyo, Badru amefafanua kuwa, endapo bajeti isingeongezwa wanafunzi 28,000 wangekosa mikopo na kwamba waliopata walikuwa tayari wameshafanyiwa tathmini.