Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Leo Agosti 2, 2021 ameanza rasmi ziara ya Kiserikali kwa siku mbili Nchini Rwanda kwa Mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.
Akizungumza na Dar24Media katika kipindi cha Mahojiano mchambuzi wa masuala ya Uchumi Innocent Ndodyabike amesema kuwa ziara za marais baina ya nchi na nchi ni ziara zenye faida kubwa kimaendeleo ya nchi hasa katika upande wa kiuchumi
Amesema kuwa Marais wanapoenda ziara huwa wanaambatana na watu mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara kitu ambacho kinawajengea mazingira mazuri ya kukuza biashara zao kimataifa
Aidha mwanauchumi Innocent amesema kuwa mara nyingi ziara hizo pia zinakuwa na lengo la kudumisha mahusiano ya kidiplomasia hasa kwenye nyanja za uwekezaji na maendeleo ya uchumi baina ya nchi na nchi.