Hatimaye gwiji wa soka nchini Ukraine Andriy Shevchenko ametabgaza kujiuzulu nafasi ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo.achia ngazi

Shevchenko ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Chelsea na AC Milan ametangaza maamuzi ya kuachana na timu hiyo, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Shevchenko mwenye umri wa miaka 44, aliteuliwa kuwa kocha mkuu mnamo 2016 na aliiongoza Ukraine kwenda robo fainali ya Euro 2020, ambapo walichapwa mabao 4-0 na England.

Shevchenko, aliyestaafu kucheza mwaka 2012, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Ukraine akiwa na mabao 48 katika michezo 111.

Alianza kazi yake ya kucheza soka huko Dynamo Kyiv kabla ya kujiunga na AC Milan mnamo 1999, ambapo alishinda mataji matano makubwa ikiwa ni pamoja na taji la Serie A na Ligi ya Mabingwa, na Ballon d’Or mnamo 2004.

Shevchenko alijiunga na Chelsea mnamo 2006 kwa pauni milioni 30, ambapo alishinda Kombe la FA na Kombe la Ligi, kabla ya kurudi Milan kwa mara nyingine ikiwa ni kwa mkopo mnamo 2008 na Aliondoka Stamford Bridge kabisa na kujiunga tena na klabu yake ya utotoni, Dynamo Kyiv mwaka uliofuata.

Shevchenko ameorodheshwa kama mfungaji bora wa sita kwenye mashindano yote ya Ulaya na mabao 67. Akifunga jumla ya mabao 176 akiwa na AC Milan, huku akiwa mchezaji wa pili mwenye magoli mengi katika historia ya klabu, na pia ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Derby della Madonnina (derby kati ya Milan na wapinzani wao wa jiji, Inter Milan) akifunga mabao 14.

Hii ndo sababu marais kufanya ziara
Msuva afunguka, "bahati ilikuwa upande wetu"