Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania na Klabu ya Wydad Casablanca Simon Msuva amefunguka kwa mara ya kwanza, baada ya klabu yake kutwaa ubingwa wa Ligi ya Morocco mwishoni mwa juma lililopita.

Wydad Casablanca ilitwaa taji la Morocco baada ya kuifunga FAR Rabat mabao mawili kwa sifuri mwishoni mwa juma lililopita, na kufikisha alama 67 mbele ya Raja Casablanca yenye alama 59, huku ikisaliwa na mchezo mmoja.

Msuva ambaye alisajiliwa Wydad Casablanca mwanzoni mwa msimu 2020/21 akitokea Difaa Hassan El-Jadeed amesema: “Ni heshima kubwa sana kwangu kunyakua taji la ligi kuu ya Morocco kupitia timu yangu ya Wydad Casablanca ninayoichezea huu ni msimu wangu wa kwanza, kiukweli ligi ilikuwa na ushindani mkubwa, lakini bahati ilikuwa upande wetu,”

“Nilitamani nifunge zaidi ya mabao saba niliyomaliza nayo msimu, hata hivyo si mbaya kwani nilipambana kuwa katika kikosi cha kwanza, licha ya kuwakuta wachezaji ambao walikuwa wanaaminiwa na wanaushindani wa hali ya juu ambao niliuchukulia kama chachu ya kujituma zaidi,”

“Mtazamo wangu umekuwa wa kuangalia mbali zaidi kuhakikisha nafanya makubwa ambayo yatakuwa alama kwa wengine kujifunza kutoka kwangu na najua wapo ambao wanajifunza hadi leo.”

Shevchenko aibwaga Ukraine
Waziri Mkuu atembelea bandari ya Kyela, Mbeya