Wabunge wamepinga Kiwanda cha Saruji cha Twiga kununua hisa za Kiwanda cha Saruji cha Tanga wakati wa uchangiaji hoja kwenye hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Wakati Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Nyimbo (CCM) akimshauri Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kuliangalia kwa makini jambo hilo ili lifanywe kisheria, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Ezra Chiwelesa yeye aliishauri serikali izingatie taratibu katika mauzo ya hisa.

Mbunge wa Mkinga, Dastan Kitandula yeye alisema wananchi wa Tanga hawataki kuona Tanga Cement ikitaifishwa wakati Mbunge wa Misungwe, Alexander Mnyeti akiishauri serikali ilinde wawekezaji wa ndani.

Naye, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby alisema: “Tunachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha je, kiwanda kitafanya kazi baada ya kuuzwa? Wafanyakazi hawatapoteza ajira zao? aliuliza huku Mbunge wa Bunda Vijijini, Mwita Getere akisema Kiwanda cha Saruji Tanga ni mali ya wananchi.

Hata hivyo, Wabunge hao waliishauri serikali ihakikishe viwanda vyote vilivyobinafsishwa na havifanyi kazi vinarejeshwa serikalini ili wapewe watu wengine ambapo Mbunge wa kuteuliwa, Riziki Lulida alisema viwanda vingi vilivyobinafsishwa havifanyi kazi.

Real Madrid wanatoa JIWE wanaweka CHUMA
Wingu la madhila kwa Waandishi, vyombo vya Habari