Fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2021) zitaandika historia mpya baada ya kukamilika kwa michezo ya kuwania kufuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Cameroon mwaka 2022.
Fainali hizo zitashirikisha mataifa sita kutoka ukanda wa wa Mataifa ya Kiarabu, baada ya kujihakikishia kufuzu, kwa kupata alama za juu kwenye makundi.
Mataifa hayo ni Algeria, Morocco, Tunisia, Misri, Mauritania, na Sudan huku Libya wakikosekana kwenye orodha hiyo, kufuatia kufanya vibaya kwenye michezo ya kundi J.
Pia fainai hizo zitashuhudia kukosekana kwa timu kutoka ukanda Afrika Mashariki, baada ya mataifa manne kutoka ukanda huo kufuzu kwenye fainali zilizopita (AFCON 2019) zilizofanyika nchini Misri.
Mataifa yaliyofuzu ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Comoros, Equatorial Guinea, Ethiopia, Gabon na Gambia.
Mataifa mengine ni Ghana, Guinea, Guinea Bissau, Ivory Coast, Malawi, Mali, Mauritania, Misri, Morocco, Nigeria, Senegal, Sudan, Tunisia na Zimbabwe.