Serikali ya Saudi Arabia imeandaa ofa kubwa zaidi katika historia ya soka la nchi hiyo ili kumnasa Nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Dunia, Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi.
Matajiri hao wanataka kutengeneza historia mpya kwenye ligi ya Saudia, wakitaka kuwa na miamba miwili ya soka duniani, akiwemo Cristiano Ronaldo anayecheza Al-Nassr FC.
PSG, huenda ikawa bila Messi msimu ujao baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kutofanyika hadi sasa, huku tetesi zikidai PSG ina mpango wa kupunguza mastaa kwenye timu yao.
Kama dili la Messi litatiki basi anaweza kulipwa Pauni milioni 320 kila mwaka, karibu mara mbili ya Pauni milioni 165 anazolipwa Ronaldo.
Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu 2022/23, huku baba yake mzazi Jorge, akiripotiwa kuiarifu klabu hiyo ya Ufaransa kuhusu uamuzi huo mwezi mmoja uliopita.