Mlipuko wa Homa ya Nguruwe ulioikumba India umesababisha vifo vya watu 1,094 kwa kipindi cha miezi minane iliyopita huku ikisemekana kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi na unasambaa kwa kasi zaidi.
Idadi ya watu waliofariki kwa mwaka huu ni mara nne zaidi ya idadi iliyoripotiwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2016 ambapo maambukizi ya ugonjwa huo yalikuwa yameshuka sana.
Aidha, katika Jimbo la Maharashtra lililopo magharibi mwa nchi hiyo ndilo lililoathirika zaidi ambapo waliofarikini kutokana na ugonjwa huo ni takribani watu 437 kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya nchini humo
Hata hivyo, Mlipuko mbaya zaidi wa homa hiyo ambao uliikumba nchi hiyo ulitokea miaka ya 2009-2010, ambapo watu 50,000 waliambukizwa na wengine 2,700 kufariki dunia kote nchini humo.
-
UN yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Syria
-
Qatar yawatimua wanadiplomasia wa Chad
-
Korea Kaskazini yafyatua makombora mengine, Marekani yapuuza
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Matibabu katika hospitali ya  Shanthi ambayo ni ya binafsi, Dkt Sanjay Gururaj, amesema kuwa si lazima kwa hospitali za binafsi kutoa ripoti ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo Serikalini.