Qatar imeamuru kufungwa kwa ubalozi wa Chad nchini humo na kutoa masaa 72 kwa wanadiplomasia hao kuondoka nchini humo, huku ikirejesha mahusiano kamili ya kidiplomasia na taifa lenye nguvu ukanda wa nchi za kiarabu la Iran.

Qatar imefikia hatua hiyo mara baada ya Chad kujiunga na baadhi ya mataifa ya Kiafrika ambayo yalijitosa kwenye mzozo wa mataifa ya falme za kiarabu dhidi ya nchi hiyo kwa kutaka kuwafukuza wanadiplomasia wa Qatar  kutokana na mgogoro wa nchi hizo za kiarabu.

Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema kuwa imefikia uamuzi huo mara baada ya Chad kuonyesha dhahiri kuwa ina nia ya kujiunga na kampeni ya usaliti wa kisiasa dhidi ya taifa hilo kama mataifa mengine yaliyoitenga kwa sababu zile zile za madai ya kufadhili vikundi vya kigaidi.

Hata hivyo, Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar ambazo kwa pamoja zilikuwa zikuwaunga mkono waasi waliomuondoa aliyekuwa Rais wa Libya, Muammar Gaddafi mwaka 2011 nchini Libya, sasa zimekuwa ni maadui wakubwa katika uwanja wa mapambano kwa maslahi tofauti katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Kikwete awataka wabunge chama tawala kuikosoa Serikali
Korea Kaskazini yafyatua makombora mengine, Marekani yapuuza