Rafiki yangu, Mwanabalagha Maundu Mwingizi alipata kusimulia kisa hiki cha mwaka 1657, akisema Mtaalamu wa hesabu toka Taifa la Kifaransa, Blaise Pascal aliwahi kumuomba radhi rafiki yake kwa kumuandikia Barua ndefu sana.

Katika andiko lake, Blaise alimuambia rafiki yake kwamba, “Nimeandika barua ndefu namna hii kwa sababu sikuwa na muda wa kukuandikia Barua fupi.”

Rafiki yake alijiuliza imewezekanaje akapata muda wa kuandika barua ndefu halafu akashindwa kuandika barua fupi?, jambo hili lilimkanganya sana.

Lakini pia Maundu akaja na Hadithi ya pili, kwamba siku moja Mwanafunzi mmoja alimuuliza swali Seneta wa Marekani aliyefika Shuleni kwao kwa mazungumzo akisema, “Mheshimiwa Seneta, huwa inakuchukua muda gani kuandaa hotuba?”

Seneta akajibu, “inategemea na muda. Kama utataka hotuba ya dakika kumi na tano, nitahitaji wiki mbili kuiandaa. Kama utataka hotuba ya dakika tano, nitahitaji wiki nne kuiandaa. Na kama utataka hotuba ya saa zima, naweza kuanza (Kuhutubia) muda huo huo.”

Mwanafunzi yule naye alipigwa na butwaa, Inawezekanaje kutumia muda mwingi zaidi kuandaa hotuba fupi, lakini ikatosha kutumia muda mchache kuandaa hotuba ndefu? Jambo hili pia lilimkanganya sana yule Mwanafunzi.

Binafsi nami pia nilikuwa nashangaa inawezekanaje, lakini leo nimethibitisha ni kwanini Blaise Pascal aliandika vile na kwanini Seneta wa Marekani naye akapita njia ya Blaise kwa mimi pia kushindwa kuandika barua fupi na urahisi wa andiko refu la kumbukizi ya miaka 25 ya kuzaliwa kwa DataVision na taratibu za maandali ya hotuba yake zinavyokanganya.

Maana kiukweli tunakosa maneno na namna nzuri ya kuandika kwa urefu na kwa ufupi andiko kutokana na ukubwa wa DataVision International Limited, jinsi ilivyoleta mageuzi makubwa nchini katika nyanja za tafiti, miradi, kuyagusa maisha ya Watanzania kiujumla nk.

Happy Birthday DataVision International Limited,” miaka hii 25, imetoa somo Kimataifa na karibuni kutazama matukio machache wakati wa kusherehekea siku hii ya kuzaliwa katika Picha zisizosema maana zinahitaji wiki nne kuzielezea.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 28, 2023
Tonali aziingiza vitani AC Milan, Newcastle Utd