A. Zawadi Mauya
Aliweza kutumia vizuri second ball na kuipatia Yanga bao la kuongoza. Comb yake na Mukoko ilikuwa sahihi.
B. Yacouba Songne
Hakuwa tu na bahati ya kufunga. Muda mwingi Tuisila, Kaseke na Feisal walikuwa wakimtengenezea nafasi za wazi. Kwa nyakati tofauti aliweza kuongeza presha langoni mwa Simba.
C. Mukoko V Feisal
Simba wana viungo wepesi ambao wanaweza kukuadhibu kwenye OPEN SPACES. Utulivu wao uliweza kuziba njia zote na kuwafanya Miquissone, Morisson na Chama kushindwa kufanya lolote lile.
D. John Bocco
Gomes alianza na mfumo wa 4-2-3-1 kamakawaida. Bocco alisimama kama mshambuliaji wa mwisho mbele, mara zote tunategemea mipira imfikie ili afanye maamuzi mazuri kwao lakini haikuwa hivyo ?
E. Benard Morisson
Mara zote huwa namuona akiwa hatari zaidi pale anapotokea BENCHI. Sijajua kwanini Gomes aliamua kumuanzisha leo, Morisson hakuishi katika mfumo.
F. Tuisila Kisinda
Kasi, uwezo wa kukaa na mipira na usahihi wa kufika eneo la tukio. Hizi ni sifa zake, aliisumbua sana walinzi wa Simba na kupunguza kasi yao ?
Well done Nasreddine Nabi. Aliishi na mfumo wa 4-2-3-1 akafanikiwa.
Kuanzia style of playing “namna ya kucheza” hadi mbinu. Wachezaji walikaba njia na sio mtu.
Ubora wa Yanga ulianzia eneo la kati, zaidi alipo Mukoko na Mauya. Wao ndiyo waliamua, mipira ipite wapi na Simba wasipite wapi.
Siku hazifanani, Gomes alipotea leo. Kuanzia Team Selection “uchaguzi wa kikosi” hadi mbinu.
Kwa maoni yangu, haikuwa sahihi sana kwake kuanza na Morisson & Nyoni na kuwaacha nje Bwalya & Mzamiru.
Morisson ni mzuri akitokea benchi, namba hazidanganyi.
Gomes alibadilika kutoka 4-2-3-1 kwenda 4-1-4-1 hadi 4-3-3 lakini haikusaidia.
Pongezi kwa Yanga, Pongezi kwa Nasreddine Nabi. Leo NIMEMUELEWA.
AHSANTENI .
Imeandikwa na @jacksonsillo