Mlinda Mlango wa Simba SC Aishi Manula amewataka Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, kuufikiria mchezo ujao na kuachama na kilichotokea leo Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Manula ambaye alisimama langon mwa Simba SC kwenye wa mchezo wa leo dhidi ya Young Africans, amewasihi wanasimba kwa kuandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram).

Manula ameandika: “Alhamdulillah,
Game ilikuwa ngumu Sana tumejitahidi Sana kutafuta goal! Lakini imeshindikana hatimae tumepoteza Lakini tunamshukuru Sana MUNGU tumemaliza salama tujipange kwa Game zijazo Inshaallah!! #NguvuMoja” AirManula.

Manula anaungana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Manara ambaye ameyakubali matokeo dhidhi ya Young Africans kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Manara aliandika ujumbe huo dakika chache baada ya Mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kupuliza kipyenga cha mwisho, Uwanja wa Mkapa.

“Alhamdulillah, Tumefungwa na Team iliyocheza kimbinu vema zaidi yetu na bahati kubwa kwao,,,,”

“Hatukuwa Simba first half but hyo ndio football”. Ameandika Manara.

Licha wa kupoteza dhidi ya Young Africans, Simba SC inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa alama 73 huku watani zao wakifikisha alama 70.

Nabi afichua mbinu zilizoikwamisha Simba SC
Hongereni 'WANANCHI', Hongereni 'WANAJANGWANI'.