Taasisi ya mboga na matunda nchini (TAHA), na kituo cha utafiti wa mbegu za asili, World Vision Center (WVC) zinatarajia kuungana ili kuendeleza na kukuza sekta ya Hortculture katika ukuaji wa Uchumi nchi za Afrika Mashariki,na kuzinduliwa na Marasi wa nchi hizo .
Mkurugenzi mtendaji wa TAHA Jacquline Nkindi, amesema muungano huo utaleta tija katika jamii na taifa, amesema kuwa, kwa upande wa Tanzania sekta ya kilimo cha mbogamboga imeendelea kukua hapa nchini ambapo imepunguza kiwango cha umaskini pamoja na tatizo la utapiamlo kwa watoto.
Amesema, sekta hiyo imeweza kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa kwa kuingiza dola 779 kwa mwaka na kuchangia kukua kwa uchumi nchini.
‘’Malengo yetu katika kuendeleza sekta ya Hortculture ni kuingizia nchi zaidi ya Dolla Billioni 3 kwa mwaka na hilo linawezekana endapo tutajikita katika kutoa elimu, mafunzo na ushauri kwa wakulima wetu’’, amesema Nkindi
Aidha sekta hiyo ndiyo inaongoza kwa uzalishaji kwani zao la nyanya linazalishwa kwa asilimia 62, mananasi asilimia 59,machungwa asilimia 25, vitunguu asilimia 15 na parachichi asilimia 14.