Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 5, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi ambapo ujenzi utaanza na jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD), ili litakapokamilika huduma zianze kutolewa.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameyasema hayo hii leo Oktoba 6, 2023 Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa kiasi hicho kimetengwa ili kifanikishe ujenzi huo katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel.

Dkt. Molle alikuwa akijibu swali Namba 78 la Mbunge wa Viti Malum, Zainabu Athumani Katimba aliyetaka kujua ni lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa.

Hata hivyo, amesema ujenzi huo utaanza Januari 2024 ili wananchi wa Kanda ya Magharibi na mikoa jirani waweze kupata Huduma za afya kwa wakati.

Vision 2030 kugusa maisha ya Mtanzania wa kawaida
Wanajeshi, Maofisa wa Magereza wafutwa kazi