Zaidi ya wanajeshi 60 na Maafisa wa Magereza wamefukuzwa kazi nchini Guinea, kufuatia uvamizi wa jela uliofanyika Jumamosi huku Kiongozi wa zamani wa kijeshi, Moussa Dadis Camara, na wengine wawili wakikamatwa na kurejeshwa gerezani baada ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Serikali la RTG, limesema Maafisa waliofukuzwa kazi ni pamoja na Claude Pivi, Moussa Thiegboro Camara na Blaise Goumou na hadi sasa, mtoro Claude Pivi hajulikani alipo.

Kiongozi wa sasa, Kanali Mamadou Doumbia ametoa taarifa akisema kuwa walichukua hatua hiyo kutokana na “ukiukaji wa sheria za ajira na utovu wa nidhamu”.

Hata hivyo, tukio hili limeelezwa kama jaribio la kuhujumu mageuzi ya Serikali na jeshi limeapa kudumisha utulivu.

Hospitali Kanda ya Magharibi mbioni - Dkt. Mollel
Mabaki ya chuma kwenye kitoweo yazua taharuki