Wasindikaji wa Nyama wa Marekani wa Kampuni ya Tyson Foods, wametangaza kurejeshwa kwa takribani kilogram 13,608 za vipande vya Kuku, baada ya mabaki ya chuma kupatikana katika bidhaa hiyo.

Kampuni hiyo ilisema wito wa kurejesha bidhaa hiyo unatokana na tahadhari ya juu bidhaa hiyo iliyotengenezwa katika kituo kimoja na kusafirishwa kwa wasambazaji katika majimbo tisa ya Marekani ya Alabama, California na Illinois.

Huduma ya Usalama na Ukaguzi wa Chakula ya Marekani – FSIS, imesema kuwa imepokea ripoti moja ya jeraha dogo la mdomo. FSIS inasisitiza kuwa mtu yeyote mwenye wasiwasi wa jeraha au ugonjwa anapaswa kuwasiliana na mtoa huduma ya afya.

Bidhaa hiyo yenye umbo la dinosaur iliyoathiriwa na wito wa kurejeshwa ina muda wa kutumika hadi tarehe 4 Septemba 2024 ambapo Kampuni ya Tyson iliongeza kuwa wateja ambao walikuwa wamenunua bidhaa hiyo wanapaswa kuitupa na kuwasiliana na kampuni hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa kampuni ya Tyson, mzalishaji mkubwa wa nyama Marekani kwa mauzo, kulazimika kurejesha bidhaa ambayo tayari ilishauzwa kwani Novemba 2022, Kampuni hiyo ilitoa wito wa kurejeshwa kwa nyama ya ng’ombe, baada ya kupata vipande kama kioo kwenye nyama. Mnamo mwaka wa 2019, kampuni hiyo ilirejesha rundo la kuku wake baada ya wateja kupata vipande vya raba ya bluu ndani.

Aidha, mwaka 2022 Tyson pia ilifunga viwanda kadhaa vya kusindika kuku nchini Marekani kutokana na kupungua kwa mahitaji.

Wanajeshi, Maofisa wa Magereza wafutwa kazi
Serikali yapanga kutumia shilingi tilioni 47.424