Huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio na watu wazima itaanza kutolewa juni mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)                                                                      
 
Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo katika hospitali hiyo, Edwan Liyombo wakati wa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye matatizo ya masikio.
Dkt. Liyombo amesema kuwa huduma itaanza kutolewa mwezi Juni, mwaka huu na kwamba Hospitali ya Muhimbili imeboresha miundombinu na tayari imenunua vifaa kwa ajili ya kuanza kwa huduma hiyo.
“Sisi tunaona hakuna gharama ya mtoto kuwekewa kifaa cha usikivu kwa sababu huduma hii ataitumia katika maisha yake yote na akipelekwa shule atakuwa na uwezo wa kusikia na kuzungumza, kwa kifupi atakuwa sawa kama watoto wengine ambao hawana matatizo ya kusikia,” amesema Dk Liyombo.
Hata hivyo, Dkt. Liyombo amewataka wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kusikia kuwapeleka katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma na pia amewataka kinamama wajawazito kuudhuria kliniki ili kuchunguzwa afya zao pamoja na mtoto kwa lengo la kuzuia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 13, 2017
Video: Chadema waandaa kongamano, Lowassa, Kinana, Polepole, Mbowe kuhudhuria