Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ilala, kimeandaa kongamano kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi wa Dar es salaam na wadau mbali mbali kuhusu Demokrasia na Siasa za Ushindani Tanzania.

Akitoa taarifa hiyo Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya ya Ilala, Makongoro Mahanga ameeleza kuwa kongamano hilo litakalo fanyika kesho Mei 13, 2017 linalenga kujenga ufahamu kuhusu dhana ya Ushindani wa Kidemokrasia.

“Wapo wananchi wengi ambao hawajaelewa vyema kwamba ushindani wa kisiasa siyo uadui na wala si kosa kisheria. Na kwakweli ushindani huu ni kwa mujibu wa Kikatiba na Sheria za nchi.

Mahanga amesema kongamano hilo litahudhuriwa na aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Ngoyayi Lowassa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na wadau mbali mbali.

Huduma ya usikivu wa masikio kuanza kutolewa Muhimbili
Wakenya, Wasomalia wafukuzwa tena Marekani