Mahakama nchini Argentina imewahukumu makasisi wawili wa Kanisa Katoliki la Roma kifungo cha zaidi ya miaka 40 jela kila mmoja kwa kuwanyanyasa kingono watoto viziwi katika shule ya kanisa.

Horacio Corbacho na Nicola Corradi, pamoja na muhudumu wa bustani, walipatikana na hatia ya kuwabaka na unyanyasaji katika shule ya kikatoliki iliyopo katika jimbo la Mendoza kuanzia mwaka 2004 hadi 2016.

Padre  Corbacho wenye umri wa miaka 59 alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto katika shule inayofahamika kama Instituto Antonio Provolo de Mendoz​a katika mji wa Luján de Cuyo.

Corradi, mwenye umri wa miaka 83, raia wa Italia, alihukumiwa kifungo cha miaka 42 jela, likuwa anachunguzwa kwa unyanyasaji alioutekeleza katika shule ya Verona, nchini italia miaka ya 1970, lakini hakuwahi kushitakiwa.

Hakuna mshtakiwa hata mmoja aliyetoa kauli yoyote baada ya hukumu kusomwa.

Kesi hiyo imeishitua Argentina, nchi ambayo anatoka Papa Francis, huku wengi wakilishutumu kanisa kwa kuzorota kuchukua hatua.

Baadhi ya wazazi wa waathiriwa waliokuwepo mahakamani na walionekana wakilia na kukumbatiana.

Kanisa Katoliki limekabiliwa na shutuma za unyanyasaji wa kingono wa watoto katka maeneo mbali bali duniani katka kipindi cha miongo michache iliyopita.

China yamuweka kitimoto balozi wa Marekani
Watanzania 200 huambukizwa VVU kila siku