Mwendesha mashtaka Mkuu wa pili wa Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) Fatou Bensouda, raia wa Gambia anatarajiwa kuondoka madarakani leo Juni 15, 2021.
Bensouda amepongezwa kwa kusimamia mipaka ya Mahakama ya The Hague kama Mahakama ya uamuzi wa mwisho na alikumbana na upinzani mkubwa chini ya uangalizi wake.
Katika uongozi wake wa miaka tisa, Bensouda amesimamia kesi ambazo zilikuwa na matokea chanya ikiwemo kesi ya kwanza kufafanua shambulizi la urithi wa kitamaduni kama uhalifu wa vita, lakini pia alishindwa katika kesi ya hali ya juu, dhidi ya Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo na Makamu Rais wa zamani wa Congo, Jean-Pierre Bemba.
Wakili Muingereza, Karim Khan ambaye alimtetea William Ruto katika kesi ya ghasia baada ya uchaguzi mkuu Kenya mwaka 2007 hadi 2008 ndiye anayechukua nafasi na kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) yenye makao yake The Hague