Shujaa wa maombi kutoka nchini Uganda Jimmy Obong, mwenye umri miaka 35 ameaga dunia baada ya kugongwa na mti unaoshukiwa kuwa na mapepo.

Jimmy Obong  amefariki dunia siku ya Ijumaa wiki iliyopita akiwa pamoja na mashujaa wenzake wa maombi wakimuombea John Okodi katika kijiji cha Tecwao, Alebtong.

Ben Ogwang alikuwa ameandaa hafla ya maombi kwa jamaa yake mgonjwa aliyetambuliwa kama John Okodi, ambapo alimualika Jimmy Obong kuwa miongoni mwao wakiongozwa na Mchungaji Lawrence Ajuga.

Wakati wa maombi hayo mwanamke mmoja alipagawa na mapepo kisha akaanza kuwaelekeza watu katika mti ambao ulidaiwa kuwa na mapepo yanayohangaisha familia ya Okodi.

Kisha baadaye waliamua kukata mti huo ambao ulimuangukia Jimmy Obong ambaye alifariki papo hapo.

Msemaji wa polisi katika eneo la Kyoga Kaskazini, Jimmy Patrick Okema amesema wamewakamata watu 13 kufuatia kisa hicho akiongezea kuwa uchunguzi unaendelea.

“Ni kweli tumewakamata watu 13. Maafisa wetu wa polisi walitembelea eneo la tukio na mwili wa marehemu umepelekwa katika mochwari ya hospitali ya Alebtong Health Centre IV, ukisubiri kufanyiwa upasuaji,” amesema Okema.

Serikali yawapandisha madaraja walimu 1,135
Serikali kuifanya Mwanza kitovu kikuu cha biashara EAC