Rawan Dakik, amefanikiwa kufika kilele cha mlima mrefu kuliko yote duniani, Everest, hapo jana Mei 22, 2021.
Maandalizi ya kupanda Mlima Everest yalianza Machi 29 ambapo Dakik mwenye umri wa miaka 20 alianza kutimiza ndoto yake ya kupanda milima yote mirefu kwenye kila bara.
Kabla ya kufika kilele cha Everest, Dakik alishapanda Mlima Kilimanjaro mara nne, Mlima Aconcaqua huko Amerika Kusini na Mlima Elbrus huko Ulaya.
Katika kujiandaa kupambana na hali za milima mirefu zaidi, Dakik alifanya mazoezi katika milima mbalimbali ikiwemo, Mlima Meru, Mlima Kenya, Mlima Rwenzori- Uganda pamoja na mlima wa barafu wa Kazbek huko Urusi.
Mwezi Mei mwaka 2012, Wilfed Moshi aliandika historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufika kilele cha Mlima Everest, miaka tisa baadaye, Dakik ameiandika tena historia ya nchi kwa kufika kilele cha Mlima Everest.