Shirikisho la Ngumi la Kimatifa (IBA) limeonekana kuridhia pambano la Mtanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Mkenya, Rayton Okwiri baada ya kurusha kipande cha video kuelekea pambano hilo.

Pambano hilo la Ubingwa wa Mabara uzito wa kati, litafanyika Septemba 29, mwaka huu katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam ambapo mabondia hao watacheza raundi 12 kumsaka mbabe.

Akizungumza Dar es salaam Mwakinyo alisema siku hiyo ataonyesha ubora wake dhidi Okwiri kutokana na mazoezi anayoendelea kuyafanya.

“Watanzania na wadau wa masumbwi nchini siwezi kuwaangusha kwa sababu siku hiyo itakuwa sikukuu ya taifa namna nitakayocheza kwa kiwango.

“Ninataka kuhakikisha ninafanya vizuri katika pambano hilo, hivyo nilishaanza maandalizi kwa kipindi kirefu,” alisema Mwakinyo.

Mwakinyo alieleza kuwa yupo tayari kupigana na Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’ endapo atatokea promota wa kutoa fedha atakayokubali na mpinzani kupunguza uzito.

“Kutokana na maneno mengi ya wadau wa msumbwi kujitaji kuona nacheza na Twaha Kiduku wa Morogoro, akitoea promota na kuweka fedha za kutosha ikiwemo mpinzani kupunguza uzito,” alisema Mwakinyo.

Promota wa pambano hilo, Fadhili Maogola, alisema kuachiwa kwa video ya mkanda huo kunadhihirisha kuwa pambano hilo lipo.

“Ombi kwa Watanzania ni kutoa sapoti katika kujitokeza katika pambano hilo kwa sababu maandalizi yamefikia katika hatua za mwisho huku mabondia wakijifua katika gym zao,” alisema Maogola.

Maogola alisema kutakuwa na mapambano sita ya utangulizi ambayo yatasindikiza pambano hilo, ikiwemo Halima Bandola kuzichapa na Halima Vunjabei.

Serikali yatenga Bil. 11 ujenzi wa Miundombinu
Fedha za Wadau zitatue changamoto za jamii - Dkt. Mollel