Iceland imekuwa nchi ndogo zaidi kuwahi kufuzu kucheza kombe la dunia baada ya kuwalaza Kosovo bao 2-0 na kumaliza kileleni katika kundi lao na kufuzu michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Urusi.

Iceland ambayo ilifikia hatua ya robo fainali ya mashindano ya Euro 2016 baada ya kuwaondoa Uingereza katika hatua ya 16 bora ni taifa la raia 335,000 pekee.

Hii ndio nchi ya kwanza kuweza kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia itakayopigwa nchini Urusi mwaka 2018 ikiwa na raia chini ya milioni moja.

Gylfi Sigurdsson wa Everton pamoja na Johann Berg Gudmundsson wa klabu ya Burnley ndio waliofunga mabao ya Iceland dhidi ya Kosovo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa 2-0.

Iceland sasa wameshinda mechi saba kati ya kumi walizocheza katika kundi ‘I’ na kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia.

 

Raia wa Liberia wapiga kura kumpata rais mpya
Ndugai awanong'oneza mawaziri wateule