Waratibu wa tuzo ya mpira wa dhahabu (Ballon d’Or), France Football wameendelea kutoa orodha ya wachezaji watakaowania tuzo hiyo kwa mwaka 2017.

Mshambuliaji wa Brazil na klabu ya Liverpool  Philippe Coutinho ametajwa katika orodha ya pili ya wachezaji ambayo ilitolewa saa kadhaa zilizopita.

Dries Mertens wa klabu ya SSC Napoli, naye ametajwa katika orodha hiyo sambamba na mlinda mlango wa Atletico Madrid  Jan Oblak.

Wachezaji kutoka kwenye klabu nguli nchini Hispania Luis Suarez wa FC Barcelona na Sergio Ramos wa Real Madrid ni miongoni mwa walioorodheshwa kwenye orodha hiyo.

Orodha ya tatu imetoka na jina la mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs ya England Harry Kane, pamoja na wachezaji wengine wanaocheza ligi ya EPL kama kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin De Bruyne na mlinda mlango wa Manchester United David De Gea wametajwa pia.

Mshambuliaji wa Poland na klabu ya Bayern Munich Robert Lewandowski na Edin Dzeko wa AS Roma nao wamo.

Orodha ya wachezaji waliotajwa mpaka sasa.

Neymar (PSG/Brazil), Luka Modric (Real Madrid/Croatia), Paulo Dybala (Juventus/Argentina), Marcelo (Real Madrid/Brazil), N’Golo Kante (Chelsea/France), Luis Suarez (Barcelona/Uruguay), Sergio Ramos (Real Madrid/Spain), Jan Oblak (Atletico Madrid/Slovenia), Philippe Coutinho (Liverpool/Brazil), Dries Mertens (Napoli/Belgium), Kevin De Bruyne (Manchester City/Belgium), Robert Lewandowski (Bayern Munich/Poland), David De Gea (Manchester United/Spain), Harry Kane (Tottenham Hotspur/England)  na Edin Dzeko (Roma/Bosnia & Herzegovina)

Rais wa Misri amshukuru Salah, atoa zawadi nono
IGP Sirro aagiza wafanyabiashara wakamatwe