Wizara ya Mambo ya Ndani Nchini Morocco, imesema zaidi ya watu 2,000 wamefariki na wengine 672 kujeruhiwa kutokana na tetemeko hilo, lililopimwa na idara ya jiolojia ya Marekani likiwa na nguvu za 6.8 kwenye kipimo cha rikta na lililotokea eneo la takriban kilomita 72 kusini magharibi mwa mji kihistoria wa Marrakech.
Kitovu cha tetemeko hilo linaripotiwa kuwa katika milima ya Atlas, lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi Septemba 9, 2023 na kuharibu majengo ya kihistoria ya mji huo wa Marrakech unaopatikana na milima hiyo ambapo pia Miji na vijiji katika eneo la tukio vimeharibiwa vibaya.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani wanasema Tetemeko hilo ni baya zaidi kuwahi kutokea nchini Morocco tangu mwaka 1960, ambapo watu 12,000 walifariki kwa tukio kama hilo kwa kina cha kilomita 18.5 na ni kubwa lisilo la kawaida kwa eneo hilo.
Profesa wa Uhandisi wa Miundo na Tetemeko la Ardhi katika Chuo Kikuu cha Southampton, Mohammad Kashan amesema Matetemeko ya ardhi yenye kina kirefu kwa kawaida yana uharibifu mkubwa akilinganisha matukio ya baada ya tetemeko na picha kutoka Uturuki za mwezi Februari, 2023.