Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo wilayani Hanang, mkoani Manyara imefikia 63 na majeruhi 116.

“Kati ya waliofariki wanaume ni 23 na wanawake ni 40. Miongoni mwao, watu wazima ni 40 na watoto ni 23. Kwa watu wazima, wanaume ni 14 na wanawake ni 26; kwa watoto, wa kiume ni tisa na wa kike ni 14,” amesema.

“Majeruhi ni 116 ambapo wanaume ni 56 na wanawake ni 60; miongoni mwao watu wazima ni 60 na watoto ni 56. Kati ya watu wazima 60, wanaume ni 29 na wanawake ni 31 wakati watoto waliojeruhiwa, wa kiume ni 27 na wa kike ni 29,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo kwa Taifa kabla ya kuongoza mamia ya wananchi kutoa heshima za mwisho kwenye ibada ya kuwaaga marehemu hao katika uwanja wa shule ya msingi Katesh ‘A’ wilayani humo.

Ibada ya kuwaaga marehemu iliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Manyara, Sheikh Mohammed Kadidi pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Baba Askofu Anthony Gaspar Lagwen ambaye alisema Kanisa hilo litachangia sh. milioni tano kwenye mfuko wa maafa.

Akizungumza na waombolezaji hao, Waziri Mkuu aliwafikishia salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwajulisha kuwa ametoa maelekezo kwamba Serikali isimamie kwa namna yoyote ile masuala ya wafiwa na majeruhi na kuhakikisha kuwa wote walionusurika wanahudumiwa.

Kocha Mtibwa Sugar afichua siri nzito
Mbinu wanazotumiwa wahalifu zafichuliwa