Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameewaagiza Wananchi kuheshimu maeneo ya Hifadhi huku akisisitiza kuwa  idadi ya Tembo haijaongezeka kama inavyodaiwa baadala yake idadi ya  watu ndio imeongezeka.

Amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu mwaka 1961 wakati nchi inavyopata uhuru idadi ya watu ilikuwa milioni nane huku idadi ya Tembo nchi nzima ilikuwa 300,000 ambapo kwa sasa idadi ya watu imeongezeka hadi kufikia milioni 62 huku idadi ya tembo imepungua hadi kufikia 60,000.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye  kata ya Makuyuni katika Kijiji cha Makuyuni Juu mkoani Arusha, amewataka wananchi wa kijiji hicho kuacha kulima na kujenga makazi yao  kwenye njia za  wanyamapori (shoroba) ili kuondokana na adha wanayopata kutoka kwa wanyamapori.

Ameongeza kuwa matukio ya watu kuvamiwa na wanyamapori wakali na waharibifu hakutokani na idadi ya tembo kuongezeka bali kunachangiwa  na idadi ya watu kuongezeka na kuanza kulima na kuanzisha makazi  karibu kabisa na maeneo ya Hifadhi pamoja na kuziba njia za wanyamapori 

Katika hatua nyingine Waziri Ndumbaro amezitaka Halmashauri zote nchini ambazo zinapakana na maeneo ya Hifadhi kupanga matumizi bora ya ardhi huku akiwataka  Wananchi kuacha kulima na kuanzisha makazi kwenye mapito ya wanyamapori.

Serikali kudhibiti ongezeko bei ya mbolea
Wanafunzi waliotuhumiwa kuchoma shule watiwa mbaroni