Polisi nchini Afrika kusini, imesema idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko wa lori la mafuta siku ya mkesha wa Krismasi eneo la mashariki mwa jiji la Johannesburg imeongezeka hadi kufikia watu 34, wakiwemo wafanyakazi 10 wa afya.
Lori hilo, lilikuwa limebeba gesi na liliharibika chini ya daraja la chini katika mji wa Boksburg, na baadaye liliwaka moto ambapo Jeshi la zima moto na wahudumu wa dharula walipojaribu kuzima lori hilo la mafuta ililipuka.
Kuhusu vifo vya Wahudumu kadhaa wa afya, Waziri wa Afya, Joe Phaahla amesema vilitokea wakati wakiwa kwenye maegesho ya hospitali hiyo, wengine wakikaribia kuondoka baada ya zamu zao Krishna na wengine walipokuwa wakijaribu kuhamisha magari yao mbali na moto.
Amesema, Wengine waliopoteza maisha ni wakazi waliokuwa wamekusanyika kuona lori hilo likiungua, ambapo Takriban watu 321 waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali iliyoharibiwa, ingawa wengine walihamishiwa katika Hospitali ya jiji la Johannesburg.