Kiasi cha maambukizi ya virusi vya Covid -19 ulimwenguni kimeongezeka na kufikia idadi ya walioambukizwa kuwa takribani milioni moja.
Hayo yamejiri huku rekodi zikionesha kuwa katika wiki moja iliyopita visa vingi vya virusi vya Corona vimerekodiwa ikilinganishwa na muda wa karibu miezi mitatu tangu virusi hivyo vilipogunduliwa kwa mara ya kwanza disemba 2019.
Hadi kufika sasa bara la Ulaya ndilo kitovu cha virusi vya Corona ambako mataifa ya Italia na Uhispania yameathirika zaidi kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa COVID-19.
Hata hivyo kumekuwa na ishara ya kupungua kiwango cha maambukizi nchini Italia kutoka asilimia 18 hadi asilimia 5 ya visa vinarikodiwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.