Wakati dunia ikiendelea kukabiliana na kusambaa kwa virusi vipya vya corona (Covid-19), takribani watu milioni 10 wameripotiwa kupoteza kazi zao nchini Marekani pekee.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kazi ya Marekani, ndani ya kipindi cha wiki mbili tu zaidi ya watu milioni 6.6 waliwasilisha maombi ya kulipwa stahiki za kutokuwa na ajira.

The New York Times limeeleza kuwa duniani kote hali ni tete kwenye sekta ya ajira. Limetoa mfano wa nchini Hispania, ambapo zaidi ya watu 800,000 wamepoteza ajira zao mwezi Machi pekee. Hispania imeripoti visa vya corona zaidi ya 110,000.

Hadi sasa zaidi ya visa milioni moja duniani kote vimeripotiwa. Marekani ambayo awali ilikuwa ikiamini ina uwezo wa hadi 85% wa kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo, inaripotiwa kuwa katika wakati mgumu wa kutoa huduma ya afya.

Nchini Tanzania, hadi sasa visa 20 vimeripotiwa na mtu mmoja amepoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Idadi ya waathirika wa Corona yafika milioni 1 Duniani
Mabasi ya wanafunzi rukhsa kubeba abiria