Mamlaka ya jimbo la Guerrero, imearifu kuwa idadi ya watu waliofariki kufuatia Kimbunga Otis, kilichoupiga mji wa mapumziko wa Acapulco nchini Mexico imeongezeka hadi kufikia karibu watu 100.

Kimbunga hicho kilichopiga kwa kasi ya kilometa 266 kwa saa Oktoba 25, 2023, kilisababisha mafuriko makubwa yaliyopelekea uharibifu wa majumba, Hoteli na Biashara zingine huku magari yakizama na huduma ya umeme na mawasiliano kutatizika.

Mwanaume mmoja akipita juu ya mabaki ya nyumba huko Acapulco bay. Picha ya David Guzman.

Wakati hayo yakijiri, tayari vitendo vya uporaji vimeripotiwa katika jiji hilo lenye wakazi takriban 900,000 ambao wanakabiliwa hadi sasa na uhaba wa bidhaa muhimu kama chakula na maji safi, licha ya Serikali kuongeza idadi ya Polisi.

Awali, Idara ya kitaifa ya hali ya hewa iliarifu kuwa jimbo la Guerrero ambako upo mji wa Acapulco pamoja na jimbo jirani la Oaxaca huenda ukaathiriwa na mvua za kuanzia sentimita 20 hadi 40 na Otis kuwa na uwezekano wa kukumbwa na mafuriko hasa kwenye maeneo ufukwe, pamoja na mawimbi makubwa.

Aziz Ki afichua siri ya mabao Young Africans
Vijana 50 CCM wawezeshwa kupata mafunzo ya Uongozi