Kimbunga kikali cha majira ya baridi kimeyakumba majimbo kadhaa nchini Marekani na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 18 na kuwaacha mamia kwa maelfu wengine bila nishati ya umeme. 

Taarifa kutoka jiji la New York,  lenye upepo mkali ulioambatana na theluji, zinasema idara za uokozi zimezidiwa uwezo kushuhghulikia dharura na uwanja wa ndege wa kimataifa kwenye mji huo, umefungwa kwa muda hadi kesho Jumatatu. 

Mmoja wa raia nchini Marekani Akita amejifunika blanketi kujikinga na baridi kali. Picha ya India Post.

Aidha, Maafisa nchini humo wamesema vifo vingi vimetokana na baridi, ajali za barabarani, kuanguka kwa miti na athari nyingine zilizosababishwa na kimbunga hicho ambacho kilitolewa tahadhari ya mapema.

Hata hivyo, Majimbo mengine yaliyoathirika ni pamoja na Tennesee, Pennsylvania, Carolina Kaskazini, Ohio, Vermont na Kentucky na matatizo makubwa yaliyojitokeza ni kukosekana kwa umeme kwenye maelfu ya makazi.

Ukraine yawaonya raia wake mashambulizi ya Urusi
Mchungaji ambaka shangazi wa mchumba wake, asakwa na Polisi